GPS TRACKER NI NINI?
IJUE GPS TRACKER - 0746373222.
GPS TRACKER NI NINI?
GPS tracker kirefu chake ni Global positioning Satellite Tracker....Yani ni ufuatiliaji wa kitu au vitu vilivyo Ktk uso wa dunia popote kilipo.
Ni ufuatiliaji unaotumia satellite ya Dunia.Sote tunajua kua ktk ulimwengu juu angani wataalamu walishaweka satellite yan kifaa ambacho kinaitazama Dunia kutoka juu....Kifaa ambacho kinapiga picha ktk dunia kwa kutokea juu angani.
Internet inaposhirikiana na Satellite vinaweza kutambua kifaa fulan kinachotumia network kipo SEHEMU Gani na pia kuonesha picha halisi ya maeneo kilipo km miti,barabara,majengo,bahari na nk.....
Gps tracker ni Kifaa ambacho ndani yake kinawekwa chiep yani laini ya simu ya mtandao Fulani na baada ya hapo kifaa hiki hufungwa au kuwekwa ktk sehem yenye umeme wa DC power ili kifaa hiki kiwake na kufanya kazi sawa na SIMU inavowaka na kufanya kazi.
DC Power ni umeme ambao sio wa moja kwa moja toka Tanesco yani ni umeme ulioondolewa mawimbi ya umeme kwani sote tunajua vifaa vyote vya electronics vina mfumo ambao hubadili umeme wa tanesco yani A.c current na kuwa D.c current na malengo ni kufanya vifaa vya ndani visiungue.
Gps tracker unaweza kufunga kwa MAGARI,PIKIPIKI,MELI,BAJAJI,BOTI,RADIO,TV,JENERETA NK.....
Kifaa hiki kikifungwa ndani ya vyombo vya moto hukuwezesha kufatilia chombo hiko Cha moto mahali POPOTE kinapoenda na utafatilia kupitia simu janja Yani Smart phone au kompyuta ya kawaida ambayo uta download app iliyounganishwa na Gps husika....
Jambo hili huwezesha kukamata chombo kilichoibiwa kwani kupitia Gps tracker utaona speed ya chombo cha moto inavotembea,kuzimwa na kuwashwa kwa chombo,mitaa na barabara zote na mengne mengi.....
Pia zipo Gps kwa ajili ya kufatilia wanyama mfano porini,askari wa wanyama pori huwafunga vifaa hivi wale wanyama wenye thamani kubwa ili kufatilia walipo na kujua usalama wao dhidi ya majangili wanaowinda wanyama BILA vibali.
Kwa mahitaji ya kufungiwa GPS TRACKER katika MAGARI,PIKIPIKI,BAJAJI,BOTI,MELI,JENERETA,TV,RADIO Nk.....Usisite kutupigia simu 0746373222 au 0657396880.
Pia tunapatikana mitandao ya kijamii Kwa majina haya.
Facebook; Gordon Technology
Instagram; Gordon_technology
Twitter; Gordon technology
Email; thedon91harrison@gmail.com
Whatsapp: 0746373222.

Comments
Post a Comment